Mihemko! Tazama jinsi Awiti wa 'The Real House help' alivyabirikiwa kwa umbo

NA NICKSON TOSI

Awiti ni muigizaji maarufu wa filamu ya humu nchini 'The Real House help of Kawangware', filamu inayoangazia maisha ya mfanyikazi wa nyumbani na maisha katika mitaa ya mabanda nchini.

Muigizaji huyo ambaye jina lake halisi ni Winnie Rubi anamfahamika tu kama Awiti na mashabiki wake.

Hapa tumekuandalia picha za kichuna huyo ambazo kama hauna wako, basi zitakuacha kama unatokwa na mate bureee!,tazama.

Kuna uvumi kwamba Awiti na mumewe walitengana na kwa sasa, kwa sasa haijulikani kama ana mtu ama bado yuatamba uwanjani tayari kunyakuliwa na mafisi wanaotafuta warembo.

Awiti alisomea katika shule ya wasichana ya St Teresas na kujiunga na chuo kikuu cha Zetech ambapo alisomea shahada katika maswala ya Ustawi wa jamii na Utumishi wa jamii.