logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mama’s Boy! Diamond Platnumz achora tattoo za jina la mamake katika mkono wake

Mama’s Boy! Diamond Platnumz achora tattoo za jina la mamake katika mkono wake

image
na

Habari02 October 2020 - 05:57
Diamond Platnumz   hivi karibuni amekuwa akionyesha tattoo katika mkono wake wa kushoto. Tatoo hiyo ni ya jina la mamake, Sandra .

Msanii huyo wa Tanzania  amekuwa katika uhusiano na wanawake wengi lakini hakuna aliyewahii kuuteka moyo wake ili kustahili kuchorwa kwa vyovyote katika mwili wake, lakini  Diamond sasa amedhihirisha jinsi anavyomuenzi mama Dangote .

Amekuwa na tattoo hiyo kwa miaka mitatu sasa na hivi karibuni Mamake walionyesha picha za  tattoo hizo na kuandika ;

CHAKUDEKA MTOTO WA MAMA ALHAMDULILLAAH   ASANTE KWA ZAWADI HII @DIAMONDPLATNUMZ

Diamond ana michoro mingine kadhaa ya tattoo katika mwili wake  na moja katika kifua chake inasoma  ;

I BELIEVE IN GOD.

Katika mkono wake wa kushoto  ameweka  herufi N,T,N  na D  ambayo ni majina ya watoto wake; Nillan, Tiffah, Naseeb,  na Dylan.

Pia ana michoro ya tatto ya tarehe mbili spesheli kwake moja ni siku yake ya kuzaliwa  2-10-1989  na nyingine iliyoandikwa kwa kiroman ni siku ya kuzaliwa kwa mamake; 7-7-1967.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved