Msanii wa bongo TID afutilia mbali uvumi kuwa anamchumbia Huddah Monroe

TID
TID
Msanii wa nyimbo za bongo TID almaarufu Khalid Mohammed  amekana madai kuwa anamchumbia Huddah Monroe, akiwa katika mahojiano na runinga ya ‘s FNL Show alizungumza na kukataa uvumi huo ulioenea sana katika mitandao ya kijamii.

Msanii TID ailfahamika sana kwa wimbo wake wa 'Nyota yako' ni kibao ambacho kilienea sana katika mitandao ya kijamii.

TID alikuwa na ujasiri mwingi sana alipokana uvumi wa kumchumbia sosholaiti wa Kenya Huddah huku akisema kuwa hawajawahi kutana hata siku moja.

Alikuwa na haya ya kusema,

“Huddah hata sijawahi kukutana naye tena sasa hivi akitaka tukutane nakuja nimejifunika kuna Covid 19.” TID Alisema.

Uvumi huo wa TID ulitokea tu baada ya msanii mwenzake Juma JUX pia naye kuambiwa anamchumbia Huddah baada ya picha zao wakiwa Zanzibar kuenea katika mitandao ya kijamii.

Juma alisema kuwa ni marafiki. Kati yake na Huddah hamna kitu kingine, huddah kwa muda hajakuwa akifichua wanaume ambao amekuwa na uhusino na wao.

Lakini mwezi jana mwanasosholaiti huyo alifichua kuwa hajawahi kuwa hana mchumba katika maisha yake.