https://twitter.com/dianamarua_/status/1256220183884169219
Lakini hakujua kwamba atageuziwa mtutu wa bunduki na kuanza kujitetea akikimbia kuitetea hadhi yake baada ya kuibuka madai kwamba wakati mmoja alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwanasoka Victor Wanyama. Madai hayo yalianzia twitter na picha zikaambatanishwa na madai hayo .
Katika youtube, wakati wa maswali na majibu ambapo alijumuika pia na mumewe Bahati Diana amesema hakuwahi kuwa katika uhusiano na mchezaji huyo wa soka na kwamba walikutana kupitia kwa rafiki yao mmoja.
“ Nilikutana na Victor kupitia kwa rafiki na tukajivinjari kwa muda na ndiposa zilipigwa zile picha’
Diana pia amewalaumu KOT kwa kuanzisha madai hayo akisema waliamua kuzitumia picha za selfie pekee badala ya picha walizopigwa kwa makundi wakiwa watu wengi .
Bahati alikuwa kimya wakati mke wake akijitetea na kujaribu kuvunja madhara ya uvumi uliokuwa umesambazwa na wanamitandao.
Bahati huenda ndiye akajilaumu kwa makombora ambayo mkewe anarushiwa kwani mwezi jana aliibuka na posti ya dharau kwamba hakuna mwanamume anayeweza kumtunza mke wake kwa sababu ni wa hadhi ya juu. Madai hayo ndio yaliyowachemsha wanamitandao waliozama na kuibuka na picha hizo za jadi za Diana ili kumpa adabu Bahati kwamba kulikuwa na wanaume wengi mbele yake katika maisha ya Diana kabla hajakutana naye.
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO