Katika video ndefu aliotuma mitandoni, Betty Kyallo pia alijipata akifichua baadhi ya vitu ambavyo yeye hufanya akiwa mlevi kama vile kuwapigia simu wapenzi wake wa zamani. Amesema amekuwa akifikiria kuhusu uwezekano wa kujitosa tena katika ndoa baada ya kutalakiana na Denis Okari. Anasema wakati walipoachana na Okari, hakutaka tena kufikiria kuhusu ndoa lakini muda umemponya na kweli sasa ameanza kujifikiria kama mke wa mtu kwa mara nyingine tena.
“Kwa muda mrefu sikuwa nimefikiria kutaka kuolewa lakini sasa najua kilichofanyika na nafahamu naweza kuboresha kipi, najua ninachofaa kutafuta kwa mwenzangu," alisema.
Kuhusu kupata watoto alisema angetamani mtoto wake Ivanna kuwa na wenzake .
“ Kwa kweli ningependa kuwa na watoto zaidi kwa sababu itafika wakati iwapo sitampa Ivanna kaka au dada ataniambia ‘mama zungumza na mkono wangu kwa sababu sikusikilizi’ alisema Betty.
Mapema mwaka huu, rafiki yake Okari Ken Mijungu alipasua mbarika kwamba Betty alikuwa katika uhusiano na mwanamume mwenye asili ya kisomali ambaye mtangazaji huyo amemficha kutoka macho ya umma na mengi hayajulikani kumhusu.
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO