'Kuja Konde Gang!' Harmonize amwambia Rich Mavoko baada ya kutoka WCB

Wasanii wa nyimbo za bongo Harmonize na Rich Mavoko walikuwa wamesajiliwa katika lebo ya WCB, ambapo walitoka katika lebo hiyo kila mmoja kwa wakati wake.

Ni wazi kuwa wawili hawa hawako katika uhusiano mwema na msanii mwenzao Diamond.

Wiki iliyopita, Harmonize alifichua jinsi Rich Mavoko alinyanyaswa na lebo hiyo alipokuwa anatoka. Mavoko alitoka kwenye lebo hiyo mwaka wa 2018.

Mwaka jana, Harmonize alifuata mkondo uo huo, licha ya kuwa mkataba wake haukuwa umeisha. Aliambiwa alipe mamillioni ya pesa ili aweze kuruhusiwa kutoka katika lebo hiyo.

Baada ya hapo, Harmonize alianzisha lebo yake inayofahamika kama' Konde Gang' na anamualika Mavoko ajiunge na lebo hiyo.

“HAVE YOU EVER THOUGHT HOW RICH MAVOKO’S MOTHER FEELS WHEN YOU TALK ABOUT HIM IN A NEGATIVE WAY?”

AS YOUR BROTHER, I’D LIKE YOU TO KNOW THAT YOUR SILENCE MEANS A LOT. WE LOVE YOU AND WE PRAY FOR YOU. LETS GO BROTHER, AS YOUR YOUNGER BROTHER, I’M HERE FOR YOU." Ujumbe Ulisoma.

Msanii huyo akiwa kwenye mahojiano na Cloud fm alisema hana shida yeyote kumsajili Mavoko kwa lebo yake kwa maana alikuwa kielelezo chake chema katika siku za awali.

“I LEARNT MUSIC THROUGH HIM AND I KNOW HIS CURRENT SITUATION AND LIFE RIGHT NOW. I DON’T KNOW HIS PROBLEMS BUT EVERY ARTISTE HAS HIS OWN PLANS. BUT I AM HURT WHEN I SEE PEOPLE SPEAK NEGATIVELY ABOUT HIM

RICH IS MY BROTHER AND HE IS TALENTED AND IF THERE IS THAT OPPORTUNITY TO WORK WITH HIM, WHY NOT?”

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO