Kenya imefikisha watu 1161 walioathirika na virusi vya Corona - Mutahi Kagwe

EYnpqw8XQAAItN4
EYnpqw8XQAAItN4
Waziri wa afya amesema chini ya saa 24, wagonjwa 52 walioambukizwa virusi vya corona nchini wamepatikana  baada ya kuwafanyia watu 2,567 vipimo.

Kati ya visa hvyo vipya 52 , watu saba wametoka katika kaunti ya Busia huku eneo la Kibra katika kaunti ya Nairobi  likisajili visa 8 hali ambayo imeanza kuipa serikali kiwewe kuhusiana na ongezeko hilo.

Kwa ujumla, Nairobi imesajili visa 23 kati ya hivyo 52.

Kaunti ya Mombasa kwa mara ya kwanza imesajili visa vichache zaidi ikiwa imesajili visa saba.

Ameongeza kuwa wagonjwa watano zaidi wameruhusiwa kutoka hospitalini baada ya kutibiwa na kupata nafuu na kufikisha idadi ya watu waliopona nchini kuwa watu 380.

Ameongezea kuwa kufikia sasa wahudumu wa afya takriban 11,000 wamepewa mafunzo maalum ya kukabiliana na vitrusi hivyo kutoka kwa kaunti zote 47 nchini.

Mutahi amewashauri madereva wote wa masafa marefu kuzingatiua masharti yaliyowekwa na serikali kwa kusubiri kufanyiwa vipimo kabla ya kuanza safari.

Akitilia podo swala hilo,  gavana wa Machakos Alfred Mutua amesema watawazuilia madereva wote ambao hawatakua na cheti cha kuonyesha hali yao ya afya.

Akihutubia taifa kuhusiana na takwimu za kila siku kuhusianan na corona, Mutahi amesifia pakubwa juhudi ambazo zimepigwa na magatuzi yote nchini akisema ni dhahiri kuwa maendelea sasa yamewafikia wananchi.

Mutahi amesifia pakubwa miundo msingi iliyowekwa kwa kaunti ya Machakos haswa kuhusiana na hospitali akisema ni sharti sasa wananchi watumie fursa hiyo kuanza kutathmini hali yao.

Wizara ya afya pia imekabidha serikali ya kaunti ya Machakos vifaa vya kufanikisha kazi ya wahudumu wa afya .