Maafisa hao ambao wamezuiliwa na idara ya ujasusi nchini DCI wanatarajia kufikishwa mahakamani hapo kesho kujibu madai ya wizi wa pesa za umaa.
Waliotiwa mbaroni ni Jacqueline Njeri Kangiri ambaye ni Meneja mkuu wa KEBS kaunti ya KIsumu japo akahamishwa hadi Nairobi ,Catherine Nangila Wanyonyi ambaye alikuwa nafanya kazi katika idara ya kutathmini biashara eneo la Kisumu na wote kutiwa mbaroni Ijumaa.
Wengine ni Linet Bitengo Nyanchama na Daniel Ambrose osumba ambao wote walikuwa wahasibu wa pesa.
Wanne hao sasa watafikishewa katika mahakama za Kisumu kujibu madai ya ufisadi dhidi yao hya kuiba shilingi milioni 12 walipokuwa wanahudumu katika matawi ya KEBS kaunti ya Kisumu kati ya mwaka 2017 na 2018..
DCI sasa imeanza mcahkato wa kuwatafuta watu wengine watatu ambao wanakumbwa na madai sawia akiwemo Erick Kibet Sawe ,Rose Wangui Gacheru na Florence Awino Ouma,wote waliokuwa wanafanya kazi kjatika halmashauri hiyo kaunti ya Kisumu.
Kwa pamoja watu hao saba wanatuhumiwa kewa kuiba shilingini milioni 12,791,126 kutoka kwa za KEBS .