Den Duale ,Ben Washiali na Kimani Kimani Ichung'wa wapo katika hatari ya kufurushwa katika nyadhifa za uongozi bungeni baada ya kushtumiwa kwa kutokuwa waamonifu kwa kiongozi wa chama chao cha Jubilee Rai Uhuru Kenyatta. Baada ya kufaulu kutekeleza mageuzi katika senate washirika wa rais Uhuru Kenyatta sasa wamepata ujasiri wa kuzidisha adhabu yao hadi bungeni na imeibuka kwamba mkutano wa wabunge wa Jubilee huenda ukafanyika tarehe 2 au 6 Juni .
Rais Uhuru Kenyatta analenga kunadhifisha usimamizi wa mabunge ypote ili kurahisisha utekelezaji wa jenda yake anapokaribia kumaliza muhuma wake mwaka wa 2022 . Ruto na viongozi katika mrengo wake wameshtumiwa kwa kuendeleza siasa za kumrithi rais Uhuru Kenyatta na kuhujumu jitihada za rais kutekeleza ahadi nyingi za maendeleo alizotoa kwa wakenya mwaka wa 2013 na mwaka wa 2017 . Washiali ambayeni kiranja wa walio wengi bungeni ,naibu wake Cecily Mbarire na mwenyekiti wa kamati ya bajeti Kimani Ichungwa, ni miongoni mwa wanaolengwa endapo Jubilee italenga kuendeleza msururu wa kuwaondoa washirika wa Ruto katika uongozi wa bunge.
Ingawaje jina lake limetajwa kwa wanaoweza kufurushwa kama kiongozi wa wengi bungeni ,Aden Duale amekuwa akituma jumbe za kukinzana wakati mmoja akieleza kwamba yupo nyuma ya rais Kenyatta na haijabainika endapo chuma chake kipo motoni .