Alitundika mitandaoni picha yake akiwa barubaru ( akiwa na DJ Moz mwaka 2005) ambayo kwanza iliwekwa na Willis Raburu na kuandika maelezo yafuatayo kufikisha ujumbe nyumbani.
"ASANTE @WILLISRABURU KWA KUNIKUMBUSHA UMBALI NIMETOKA !! NILIKUWA NA MIAKA 18. KAZI YA KWANZA KATIKA HOPE FM. NIKILIPWA PESA KIDOGO. WAJUA NINI CHINI YA KIDOGO? HIYO NDIO NILIKUWA NALIPWA. NINGETOKA CHUO KIKUU CHA DAYSTER ATHI RIVER, NISHUKIE AIRPORT VIEW ESTATE NA KUTEMBEA KAGUU NA NJIA HADI NPC VALLEY ROAD… KUSEMA UKWELI ILIKUWA NI KAMA NAKIMBIA! MBONA NITEMBEE LAKINI, NILIKUWA NIMECHAGUA KUTOPANDA BASI AU KUCHUKUWA TEKSI, KWA SABABU NILITAKA KUWEKA ZILE PESA ILI NITUMIE KWA NAULI," KIGUTA ALISEMA.
Anna Kiguta hatoki katika familia iliozaliwa na asali mezani bali anatoka katika familia ya walala hoi.
"KAMA WENGI WETU SIKUZALIWA KATIKA FAMILIA TAJIRI, KILE NILIZALIWA NACHO NI WAZAZI WAZURI WENYE MAADILI MEMA . NA KAMA TU FAMILIA YANGU, ILIBIDI NIFANYE YOYOTE ILE ILI KUKIDHI MAHITAJI YANGU. NA NIMEENDELEA KUFANYA HIVYO. SIO ETI TULIKUWA MASIKINI SANA KWA SABABU WAZAZI WANGU WALIWEZA KUMUDU KARO YANGU NA NILIENDA KATIKA SHULE NZURU, LAKINI LENGO LILIKUWA KWAMBA LAZIMA UTOWE JASHO ILI UPATE. NIKIANGALIA NYUMA NASEMA NI ASANTE, " ALIELEZA.
Mwanahabari huyo wa maswala ya kisiasa katika kituo cha K24 ana shukrani nyingi sana kutoka kwa Mungu kutokana na safari aliyotembea maishani. Anne Kiguta ni mojawapo wa wanahabari wa kike shupavu sana nchini kwa sasa.
Alimshukuru Willis Rabusu akisema kwamba picha hiyo inampa kumbukumbu ya maisha yake na kumpa ujasiri wa kufanya hata bidii zaidi maishani mwake. Alimuomba Mungu kuendelea kumpevusha ili apige hatua zaidi maishani.