Maafisa 8 wa polisi wanusurika kifo baada ya kambi yao kuteketezwa Naivasha

h9MMVvNf.jfif
h9MMVvNf.jfif
Maafisa wanane wa polisi wamenusurika kifo baada ya kambi yao kuteketezwa eneo la Naivasha wakati wa mandamano ya kukashifu udhalimu wa polisi.

Kisa hicho cha Alhamisi, Juni 11 asubuhi, kiliwashuhudia maafisa hao wakipoteza mali yenye thamani ya pesa.

Kulingana na wakazi, waliotekeleza kitendo hicho walianza kwa kufungia nje mlango wa afisa aliyekuwa zamuni kabla ya kuwasha gurudumu nje ya mlango wake.

Moto huo ulianza kusambaa katika nyumba zingine huku maafisa hao wakihangaika kutorekea usalama wao, moto huo ukichukua masaa mawili kuzima.

"Walikuwa wanalenga nyumba ya Inspekta ambaye hakuwepo lakini moto huo ulichoma nyumba yake kabla ya kusambaaa kwa nyumba zingine," alisema mkazi mmoja.

Inaaminika kuwa wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakilalamikia kudhulumiwa na maafisa wa polisi wa kambi hiyo jambo ambalo linasemekana lilichangia tukio hilo.