Waasanii hao wa Afrika mashariki kutoka nchini Tanzania Dar Es Salaam 255, wametoa kibao kipya ambacho kimependwa na mashabiki zaidi ya thelatini na kisha kutazamwa na watu zaidi ya millioni moja baada ya siku mbili tangu kiwe katika mitandao ya kijamii ya youtube.
Kibao hicho kinafahamika kama 'Acha Lizame', Audio ya wimbo huo ilitolewa na producer Kimambo Beats na kisha video kuelekezwa na na mwelekezi Elvis.
Wimbo wa Acha Lizame ni wimbo ambao umeimbwa kwa lugha ya kiswahili, unazungumzia kuhusu wapenzi wawili ambao wanapeana sifa kwa kila mmoja kwa wamo kwenye maabara ya mapenzi na wako tayari kufanya chochote kwa ajili ya mapenzi yao na kudumisha uhusiano wao.
Nandy na Diamond wakizungumzia kibao hicho walisema kuwa ulikuwwa umefika wakati wa kuwapa mashabiki wao ambacho wamekuwa wakitaka kwa muda mrefu.
Ni kibao ambacho kinaweza kusakatwa na kuchezwa na kila mtu nchini kote na hata dunia nzima licha ya kibao hicho kuimbwa kwa lugha ya kiswahili.
Hiki hapa kibao hicho;