D-Day :Waiguru kujua hatima yake leo

Juhudi za kumuokoa gavana wa kirinyaga Anne Waiguru zinaanza leo  anapojitayarisha kujitetea mbele  ya senate .

Gavana huyo amejipata matatani kisiasa wakati ambapo washirika wakuu kisiasa wanazingatia uwezekano wa kumnasua ingawaje hatua hiyo itakuwa pia na athari zake.

Leo senate itaamua  iwapo gavana huyo atasikizwa na jopo la wenzao 11 au maseneta wote.

Pamezuka mirengo miwili katika senate kati ya wanaotaka kumuokoa Waiguru ambao ni  maseneta wa mrengo wa rais Kenyatta na kiongozi wa ODM Raila Odinga na wanaompinga  gavana huyo walio katika mrengo wa tanga tanga unaomuunga mkono naibu wa rais William Ruto.

Baada ya kuondolewa kwa washirika wa Ruto kutola uongozi wa seneti huenda Waiguru ana nafasi ya kuweza kujiokoa kutoka shoka la kuondolewa afisini lakini hilo litathibitika tu wazi siku zijazo. Tayari chama cha ODM kimesema kitalenga kumtetea Waiguru asalie afisini