Katika mahojiano na radio Jambo Nyamweya anayelenga kuwania tena kiti cha urais wa FKF amesema kiasi kikubwa cha fedha zilizopewa FKF zimetumiwa vibaya na hapajakuwa na uajibikaji kwa upande wa shirikisho la FKF linaloongozwa sasa na Nicke Mwendwa .akitetea uongozi wake wa miaka mitano alipokuwa afisini ,amesema hakuwa akipewa ufadhili na aserikali pamoja na shirikisho la fifa kama linavyopewa fedha nyingi shirikisho la sasa .
Amemlamu mrithi wake Mwendwa kwa kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa timu ya taifa Harambee stars Bobby Williamson wakati alipochukua usukani . Nyamweya amesema mamilioni ambayo serikali inafaa kumlipa kocha wa zamani wa stars Adel Amrouche hazingetolewa endapo Mwendwa angefuata ushauri wake .
Amesema iwapo atachaguliwa kurejea afisini ataweka mazingira bora kwa wafadhili kurejea katika soka nchini .Nyamweya ameahidi kuwahusisha wadau wote wa soka kuboresha mchezo sio tu kwa soka ya wavulana bali pia soka ya akina dada .
Alipoulizwa kuhusu utendakazi wake alipokuwa uongozini alijipa asilimia 80 na kusema kwamba anahitaji nafasi nyingine kujizalia asilimia 20 iliyosalia ili kuboresha soka ya nchi .