Triple Trouble : Wasichana watatu wa shule kutoka familia moja wapachikwa mimba

teen pg
teen pg
Familia moja huko Mbeere  kusini katika kaunti ya Embu imeshindwa la kufanya baada ya wanao watatu waliokuwa   wakisoma kupachikwa mimba muda huu ambao wamekuwa nyumbani baada ya shule kufungwa kwa ajili ya janga la corona

Wasichana hao wa darasa la saba, nane na kidato cha  tatu wote walipimwa na kupatikana na mimba wakati kila mmoja wote alipoanza kuonyesha dalili za  ujauzito. Baba yao  Fred   Njuki  amesema baada ya ugunduzi kwamba binti zake wana mimba ameshinda atachukua hataua gani kwa sababu itakuwa vigumu kwake kuwatunza wakiwa na wanao. Kesi hiyo tayari ipo polisi  na wasichana hao wanazidi kuhojiwa kuwataja watu waliowapachika mimba.

Njuki amesema wameanza kutafuta misaada kutoka kwa mashirika yasio ya kiserikali ili kuhakikisha kwamba binti zake wanarejea shuleni pindi tu watakapojifungua .

Wiki jana serikali imetoa takwimu zinazoonyesha   kwamba  wasichana 4000 walipachikwa mimba wakati shule zilipofungwa  kwa ajili ya janga la corona.  wizara za elimu na afya zimeanza kuchukua hatua ili kuzuia visa hivyo huku wasichana wengi wakiripotiwa kupachikwa mimba na wenzao.