UNYAMA!Polisi wamtia mbaroni mwanamke kwa mauwaji ya wanawe wanne

Aliwaacha wengi midomo wazi na kupigwa na butwaa baada ya kukiri kuwa kuwaua wanawe wanne kwa kuwapa sumu na kisha kuwanyonga Jumamosi Juni 27. Polisi mjini Naivasha walimkamata mwanamke huyo wa miaka,42, kwa kutekeleza kitendo hicho cha unyama. Mama huyo wa watoto sita alikiri hayo kwa rafiki yake ambaye aliwaambia polisi Jumamosi jioni, kamanda wa polisi mjini Naivasha Samuel Waweru alithibitisha kisa hicho na kusema kuwa mama huyo yuko mikononi mwa polisi.

"Mshukiwa alimwambia rafiki yake kuwa wanawe wamelazwa katika hospitali ya Naivasha wakiugua kifua, baada ya saa chache alikiri kuwa aliwanyonga," Alisema Waweru.

Wanne hao walizirai wakiwa sebuleni na akawapeleka katika chumba cha kulala na kisha akatoweka kwenda mafichoni. Wawili kati ya sita hao walikuwa wameenda wakati wa kisa hicho, polisi aliyechunguza mauaji hayo alisema kuwa mama huyo alichukua muda akiwanyonga wanawe.

"Mshukiwa alichukua muda akiwanyonga wanawe na akalala na wao chumbani kimoja hadi Jumamosi asubuhi."

Kamanda wa polisi alisema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa mauaji hayo ili kubaini nini haswa kilipelekea mama huyo kuwaua wanawe.

Je wazazi wamechoka kukaa na wanao wakati huu wa janga la corona, na kitendo hicho kinahashiria nini haswa?

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO