Ogopa wanawake! ‘Nilitamani bwana ya beste yangu ,na within no time ,nilijipa’

Kuna baadhi ya wanawake wenye busara ambao kwa wakati wote wamekuwa waangalifu kuhusu rafiki zao na hasa wamekuwa wakifuatilia kwa umakini tabia za rafiki zao mbele ya waume zao ili kugundua chochote cha kuzua  shauku.

Mwanamke mmoja  amesimulia jinsi  alivyooanza kumtongoza mume wa rafiki yake na kuanza kushiriki naye mapenzi kwa lengo la kunufaika na pesa ambazo jamaa huyo alikuwa nazo. Cha Kuhuzunisha ni kwamba baada ya rafiki yake kugundua kwamba mumewe alikuwa na uhusiano wa pembeni, alitafuta ushauri wa mwanamke ambaye alikuwa katika uhusiano huo na mumewe bila kujua.