Beatrice Mwende, 42, amesema alikuwa ameingilia na mapepo na yungali anafikiri yupo kwenye ndoto baada ya kutekeleza mauaji ya wanawe na sasa anamlaumu mpenzi wake huyo waliyetangana naye mwaka jana . Mwende amesema anapitia uchungu nab ado hajaelewa kilichofanyika .Alifikishwa kortini jana mbele ya hakimu mkaazi wa Naivasha Yusuf Baraza.
Mama huyo wa watoto sita alisimulia jinsi walivyowauawa watoto wake wanne siku ya ijumaa kwa kuwapa sumu kabla ya kwenda kulala .
Mwende, mwalimu wa hesabu aliyekuwa akifanya kazi na shirika moja lisilo la serikali mjini Naivasha aliomba msamaha kwa hatua hiyo yake na kutaka ahurumiwe akisema hakujua alikuwa akifanya . “ Mpenzi wangu wa zamani alikuwa na nguvu za mapepo alizotumia kunielekeza kufanya unyama huo na kusababisha niwaue watoto wangu wanne’ alisema
“ Nataraji kwamba ndoto hii mbaya itakamilika na nitaamka niipate familia yangu katika nuzri ya afya kwa sababu siwezo hata kumdhuru nzi’
Watoto waliouawa wametambuliwa kama Melody Warigia (8), Willy Macharia (6) — wote wanafunzi wa shule ya Milimani Primary School, Samantha Njeri (4) na Whitney Nyambura (two).
Polisi huko Naivasha wameruhusiwa kumzuilia Mwende kwa siku saba ili kukamilisha uchunguzi wao .
Mshukiwa atafikishwa tena kortini Julai tarehe 6 .
Polisi watategemea ripoti ya uchunguzi wa miili ya watoto hao na ripoti wa hali yake ya kiakili .Akikumbuka uhusiano wake wan a mpenzi wake ,Mwende amedai kwamba alikuwa na nguvu za kumfanya atekeleze mambo ambayo hakutaka .
Amesema kwamba tarehe 26 ya kila mwezi alikuwa akiingiliwa na mapepo yaliyomfanya kufanya vitu bila kuweza kujithibiti . Alimtaka mungu na familia yake kumsamehe kwa mauaji aliotekeleza ya wanawe .
Mwende amesema jumamosi asubuhi baada ya kugundua alichofanya alienda naivasha kumtafuta mwanamme huyo ambaye hufanya kazi mjini Naivasha . Kupitia barua alioandika Mwende amesema alishangazwa na hatua hiyo yake na kwamba alikuwa tayari kwenda jela kwa makosa aliofanya .