Uganda? Diamond afichua siri ya kushangaza ya baba yake mzazi

Staa wa bongo Diamond Platnumz amefichua siri ya kushangaza ya baba yake mzazi, kwenye mitandao ya kijamii ya instagram kwa miaka mingi tulijua kuwa Diamond ni mtanzania ilhali baba yake ni wa kutoka Uganda.

Kwenye mitandao ya kijamii, Diamond aliposti video ya watoto kutoka Uganda wakiucheza wimbo wake wa hivi majuzi na kuandika ujumbe mfupi uliofichua siri hiyo.

Hata hivyo, hakuzungumzia mengi kuhusu siri hiyo bali alijigamba kwa kuwa baba yake ni wa kutoka Uganda huku akisema pia wanawe wawili ni wa kutoka nchi hiyo.

"UGANDA You know my dad is from there and my two kids are from there right….?" Aliandika Diamond.

Hili lilikuja kama siri ya kushangaza kwa maana msanii huyo hajakuwa akizungumzia mengi kuhusu baba yake mzazi Mzee Abdul.

Awali, Mama Dangote na Diamond walifichua jinsi mzee Abdul aiwaacha na kwenda kuishi na mwanamke mwingine huku akiwaacha kwenye umaskini tele.

Kulingana na mama Dangote, mzee Abdul hakujisumbua kuwalea wanawe na kumlazi kuacha mambo mengi ili kuhakikisha wanawe hawajalala njaa na wala hawana shida yoyote.

Licha ya hayo yote, Diamond anaweza kuwa hana uhusiano mwema na baba yake mzazi lakini huwa anatenga muda wake na kwenda kuzungumza naye.

Kama  vile tunavyofahamu mmoja wa baby mama wa msanii huyo Zari Hassan ni wa kutoka nchini Uganda ambaye amemzalia Diamond watoto wawili.