Watoto 4 waliouawa na mama yao wazikwa

funeral
funeral
Wakaazi wa Kinangop hatimaye wamezika watoto wanne walioangamizwa na mama yao mzazi wiki ililyopita.

Watoto hao Melody Warigia (8 ), Willy Macharia (6), Samantha Njeri (4 ) na  Whitney Nyambura (2 ), wamezikwa hii leo katika kaburi la pamoja.

Hotuba ya waathiriwa ilikuwa imeandikwa kwa ufupi kama njia ya kuonyesha kuwa maisha ya watoto hao yalikatizwa kighafla

 “The late met her death on the night of Friday, June 26 under unclear circumstances, shine all the way in the land of the living untill we meet again, rest in peace.”

Mshukiwa mkuu na ambaye ni mama yao mzazi Beatrice Mwende alisema kilichomfanya kuwauwa watoto hao ni shetani na mpenziwe wa zamani.

Akiwa mbele ya mahakama ya Naivasha, mwanamke huyo wa miaka 42 aliomba mahakama kumuonea huruma ila akasema yupo radhi pia kufungwa gerezani.

Mwanamke huyo alisema kuwa siku ya kutekeleza uovu huo alishikwa na mapepo chanzo ambacho kilimpelekea kutekeleza tukio hilo.