Polisi wa Lamu afungwa jela maisha kwa ubakaji wa mwanamke

lamu cop
lamu cop
Afisa mmoja wa polisi aliyekuwa akihudumu huko Lamu amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanamke mmoja  aliyekuwa amekwenda kupiga ripoti katika kituo cha polisi .

Rodgers Ouma,  mwenye umri wa miaka 28  pia atahudumia kifungo cha miaka 10 jela  kwa kutumia vibaya maamlaka yake  na  kulipa shilingi laki nne kwa  mwathiriwa kama fidia .

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma amesema  upande wa mashtaka umethibitisha kesi yao dhidi ya mtuhumiwa bila shauku  kwamba Ouma alimhadaa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 26 hadi katika nyumba yake disemba  mwaka wa 2019 na kumfanyia unyamahuo .

Haji kupitia kwa taarifa amesema   mwanamke huyo alikuwa amekwenda kuripoti kwamba mumewe alikuwa akimlazimisha kutumia tembe za kuavya mimba ilia to euja uzito aliokuwa nao .

Hakimu aliyeshughulikia kesi hiyo Allan Temba  amesema Ouma alitumia vibaya maamlaka yake kwa kuahidi mwanamke huyo kwamba angemsaidia na kesi aliokuwa amekwenda kuripoti .