Daktari wa kwanza kufa corona alifaa kufanya harusi mwaka huu

Daktari Kenya aliyeaga dunia kwa ajili ya Covid 19  alikuwa amepanga kufanya harusi mwezi novemba mwaka huu  .

Doreen Adisa Lugaliki, 38,  alikuwa  tayari keshatakiwa wafunge ndoa na mpenzi  wake Fred Mboss  mwenye umri wa miaka 45 .wawili hao walikutana mwaka wa 2017

“ Nilimpenda kwa sababu ya urembo wake  ,tabia na werevu wake .wazazi wetu walikuwa na furaha sana  tulipowamabia kuhusu mipango yetu na waliahidi kutuunga mkono’ Mboss ameliambia gazeti la The Star kwa njia ya simu .

Wawili hao walikuwa wakiingoja serikali iruhusu usafiri wa kuingia na kutoka Nairobi ili kuwtembelea wazazi wa Adisa huko Bungoma

“ Ziara hiyo ingefuatiwa na mazungumzo kuhusu mahari  kabla ya harusi ,mipango ya harusi ilikuwa ikiendelea’ amesema Mboss .

Mipango hiyo hata hivyo ilitumbukia nyingo wakati Adisa alipoanza kuugua  julai tarehe 5  na Mboss akambikimbiza katika hospitali ya  Chuo Kikuu cha Aga Khan . alipatikana na ugonjwa wa kisukari na kulazwa saa nne usiku .

Hali yake ilianza kuwa mbaya  julai tarehe 7  baada ya kupimwa na kupatikana na virusi vya corona  kisha baadaye aakahamishwa hadi kitengo cha ICU .

“ Aliaga dunia kwa sababu ya matatizo yanayotokana na COVID 19  julai tarehe 10’ familia yake iliwaarifu waombolezaji  Bungoma wakati wa maazishi yake . Madaktari waaliweza kugundua kwamba Adisa aliupata ugonjwa huo kutoka kwa mwenzake  ambaye aliambukizwa na mgonjwa katika  Nairobi South Hospital  ambako alikuwa akifanya kazi l kama mwanajinakolojia . Mboss  alisema atakosa sana safari zao walizofanya kwenda Singapore ,Dubai  na sehemu nyingine za dunia . “ Ntaikosa sana tabasamu yako nzuri  na akli zangu pevu’ amesema

Adisa awali alikuwa ameolewa na   Kituku Kinyae  mwaka wa  2007. Haijabainika iwapo walitalakiana kwa njia rasmi  .Aliwacha watoto wake pacha  Kyla Ndinda  na  Kyle Kimilu .