Letoo alithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo baada ya kufanyiwa vipimo katika hospitali moja mjini Nairobi. Akizungumza na radio jambo, mwanahabari huyo alithibitisha habari hizo na kutuhakikishia kwamba anaendelea vyema. Letoo alisema hali yake ni thabiti na kwamba haonyeshi dalili zozote za virusi hivyo.
Haya yanajiri siku chache baada ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanawe baada alipokuwaya kufikisha umri wa mwaka mmoja na kuweka picha zao kwenye mitandao ya kijamii.
Si mmoja wala wawili bali baadhi ya mashabiki wake walimpongeza na kupendezwa na picha zake na mwanawe.
Letoo ni miongoni mwa watu mashuhuri waliopatikana na virusi vya corona humu nchini, anafahamika sana kwa kazi yake ya uhanahabari katika runinga hiyo, hasa katika kuelezea masuala kuhusu janga la Corona.
Kutoka kwetu wanajambo tunamtakia afueni ya haraka.