Baada ya uzinduzi huo staa wa bongo Diamon Platnumz alimzawadi msanii Zuchu na gari lililokuwa linafanana na lile alimzawadi Tanasha mwaka jana.
Awali Zuchu alisema kuwa alikuwwa anatumia gari za abiria yaani matatu, huku nyimbo zake zikichezwa katika redio.
Diamond kupitia kwa ujumbe wwake alimwambia Zuchu awe mwwenye heshima kama Mama yake mzazi, huu hapa ujumbe wa Diamond kwa Zuchu.
"Kwa kila maisha kila kitu inawezakana ilhali tunapaswa kuamini katika ndoto zetu na kisha tuombe sana kuwa mwenye heshima na nidhamu na kutakia kila laheri Zuchu." Alizungumza Diamond.
Gari hilo lililetwa kwenye jukwaa na msanii Rayvanny ambapo Zuchu alikuwa anawatumbuiza mashabiki na wasanii wenzake huku akitiririkwa na machozi ya furaha na Diamond kumkumbatia wakati huo.
Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya instagram,Zuchu alichukuwa fursa hiyo na kumshukuru Diamond kwa kitendo hicho, na kuandika ujumbe ufuatao;
"Mwenyezi Mungu wangu nasema Alhamdulillah,Mbariki boss wangu na umuongeze kwa hiki kikubwa alichoniongezea kwenye maisha yangu.Si kila mtu anamoyo kama wako boss Hakunaaa cha kukulipa My brother hakuna kwakweli Allah akupe umri wa uhai wenye mafanikio zaidi unatuokoa wengi sana Asante boss." Aliandika Zuchu.
Tazama baadhi ya picha zao;