Njoro ambaye alikuwa akifanya kazi kwa karibu sana na marehemu Papa Shirandula amesema kwamba Papa hakuwa tu rafiki yake bali alikuwa kama kakake mkubwa .
Akizungumza na katika kipindi cha Youtube cha Jalang’o #BongaNaJalas, Njoro amesema urafiki wa papa Shirandula ulikuwa nguzo muhimu sana katika shughuli zake kikazi na hata kifamilia akiwa nyumbani .
Amesema Papa alikuwa tayari wakati wote kutuliza mambo na kutafuta suluhisho wakati Njoro alipokuwa amejipata katika mgogoro na mkewe .
“Papa was not a friend to me he was a brother to me wakati nilikuwa na mashida nyumbani nilikuwa nikipigia Papa akuje aongee na bibi yangu mambo inakamilika. Papa alikuwa anasolve shida zangu za nyumbani,” amesema Njoro
Njoro pia alisema walikuwa na uwekezaji pamoja na walikuwa wakisadiana kufungua biashara za wake zao .
“Second in terms of investments tulikuwa tunainvest na Papa tunaulizana sasa wife nikimuongezea hii project atakuwaje,” aliongeza mchekeshaji huyo