'Nimeona watu wakipoteza maisha yao kwa ajili ya shinikizo ili kufurahisha nchi-Azziad Nasenya

Malkia wa mitandao ya kijamii ya Tiktok Azziad Nasenya aliamua kueleza mashabiki wake safari yake ya kuwa maarufu kwa muda mfupi, Azziad alisema kuwa haikuwa tu kwa bahati nzuri bali kwa bidii yake alioifanya.

Kupitia kwenye mitandao ya kijamii Nasenya alifichua kuwa alikuwa anawaomba watu kumuunga mkono kwa kazi yake hadi pale alikuwa anataka kukata tamaa kwa maana hamna kitu chochoye  kilikuwa kinatendeka.

"Sitaki kujipoteza nimeona watu wengi wakiaga dunia kwa ajili ya shinikizo wakijaribu kufurahisha taifa, shinikizo ya mitandao ya kijamii ni kweli ndio maana huwa naambia marafiki zangu na marafiki wa karibu waweze kuepuka

Litakuharibu kwa maana mwishoni mwa siku hamna mtu yeyote anajali, jipende jinsi ulivyo." Azziad Alisema.