Nilijaribu kujiua-msanii wa wimbo Gold digger Jackie Chandiru afichua

Msanii  tajika wa Uganda Jackie Chandiru ambaye aliwahi kupambana na uraibu wa kutumia dawa za kulevya amerejea tena katika ulingo wa muziki .

Msanii huyo wa kibao kilichotambaa cha Golddigger  ametoa wimbo mpya kwa ushirikiano na mkenya   Arrow Bwoy kwa jina ‘ The One’.

Picha zake akiwa amechanika na  huku akikosa kujielewa ziliibuka katika vyombo vya habari nchini mwake na kutokea ripti kwamba alikuwa akitumia dawa za kulevya kama vile cocaine na heroine lakini staa huyo wa zamani wa  kundi la  Blu 3 sasa ameamua kujitosa tena katika fani ya muziki .

Amezungumza na  mpasho  kupitia instagram Live  na amekanusha kuwahi kutumia dawa za kulevya

 Nilikuwa mraibu wa kuituia dawa kwa jina  PETHIDINE;  ilikuwa dawa ya kupunguza maumivu wala sio dawa ya kulevya  na nilianza kuitumia baada ya kupata jeraha la mgongo na nilifaa kufanyiwa upasuaji ila ilikuwa ni jambo la 50-50 uwezekano wa kupoteza maisha yangu au kupona

Alifikiria kuhusu upasuji huo lakini akapatwa na hofu kwamba hangeweza kutembea

 (PETHIDINE)  ilikuwa dawa ya kunipa afueni ya maumivu haraka  na kuanzia mwanzo nilionywa kwamba ningejipata nimekuwa mraibu wa kuitumia ,baadaye nilijipata katika tatizo la kuacha kuitumia dawa hiyo  wala sikuitumia kulewa ama kwa raha ni kwa sababu nilikuwa naitumia kupunguza  maumivu

Hatua hiyo iliathiri taaluma yake katika muziki na hata akasahaulika  .Hakuwa tena akifanya muziki .

 “ utumizi wa dawa hiyo uliathiri taaluma yangu katika muziki  na ikafika wakati sikutaka kufanya kazi au kwenda studio  nilitaka tu kuwa pekee yangu  yalikuwa mambo mengine yaliyojichanganya na nikaanza kupata na mawazo kupindukia  na wakati watu walipoanza kusema mambo ya kutunga kunihusu niliamua kujifunga kabisa

https://www.youtube.com/watch?time_continue=22&v=foQ5h799PpM&feature=emb_logo

Aliendelea kusema

 nafikiri ni jambo zuri lililofanyika kwa sababu singekuwa mwanamke ambaye sasa niko hapa  hatua hiyo ilinipa nguvu na kunifunz akwamba watu wanaweza kukuinua na pia wakati mwinginme wanaweza kukukanyaga

Alipoangazia sana ,Chandiru alijipata katika matatizo mengi hasa baada ya mdai kwamba anatumia dawa za kulevya na alijaribu kujiua .

… ndio nilijaribu ,sitakanusha hilo  nilitaka kujiua  nilikuwa nimechoshwa na kila kitu  na hasa habari za wongo katika vyombo vya habari  .kulikuwa na ripoti nyingi kwamba nilikuwa natumia dawa za kulevya ilhali hata sijui cocaine au heroin zinafanana vipi