Watoto hao wawili wanadaiwa kuuwa na mwanamke jirani ambaye aliwapa machungwa yaliytiwa sumu siku ya jumatatu .mwanamke huyo amekamatwa na kiini cha kufanya hivyo hakijajulikana .
Muuguzi mmoja naye aliauawa katika nyumba za wafanyikazi wa hospitali hiyo siku ya Jumanne baadaya mume wake kumdunga kisu mara 13 kisha baadaye mshukiwa akajisalimisha kwa polisi .
Visa hivyo viwili vimewashangaza majirani .wafanyikazi wa kutoa huduma za ushauri na viongozi wa makanisa wamezua hofu kuhusu ongezeko la ghasia na dhulma za kinyumbani wakati huu wa janga la corona .
OCPD wa Gilgil John Onditi amesema jirani ya watoto hao wawili amekamatwa na andiye aliyekuwa mtu wa mwisho kuonekana nao na imebainika kwamba aliwapa sumu .
Kuhusiana na mauaji ya muuguzi aliyetambuliwa kama Josphine Kamau OCPD amesema mume wakeanayeripotiwa kuwa mkritu aliyeokoa alijaribu kujiua na alikuwa chini ya matibabu .
Onditi amesema wawili hao waligombana na mwanamme huyo ambaye ana duka la kuuza vitabu katika eneo la Nyandarua alimuua mkewe kwa kumdunga kisu mara 13.
“ Baada ya kutekeleza mauaji hayo mwanamme huyo alijaribu kujiua na anapokea matibabu kisha atafikishwa mahakamani’ Onditi amesema
Jirani ambaye hakutaka kutajwa amesema mwanamme huyo alishuku mkewe alikuwa na uhusiano na mmoja wa rafiki zake .