Amesema yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya jopo la kuchunguza mauaji ya Msando iwapo kunayo huku akiwalinganisha waliotekeleza mauaji hayo kama Judas Iscariot.
Akombe amesema kwamba maamlaka haziko tayari kukamatwa waliomwua msando hukuakiishtumu afisi ya mkurugenzi wa mashataka ya umma kwa kujikokota kuhusiana na kesi hiyo .
Siku hii miaka mitatu iliyopita mwili wa msando ulipatikana katika msitu wa Muguga huko Kikiyu katika tukio ambalo nusura lisambaratishe uchaguzi wa agosti tarehe nane mwaka wa 2017, wiki moja kabla ya kuandaliwa .
Alikuwa ameteswa na kulikuwa na majeraha katika mgongo na mikono yake kwani waliomwua walitaka awape password ya mfumo wa kupeperusha matangazo ya uchaguzi .uchunguzi wa mwili wake ulionyesha tu kwamba alikuwa na majeraha ya kukatwa lakini baadaye ilibainika kwamba alinyongwa .
Msando alikuwa ameahidi kuhakikisha kwamba uchaguzi huru na wa haki unafanyika na mfumo uliokuwa umetumie haungeweza kudukuliwa kwani ni yeye pekee aliyekuwa na password ya mfumo huo .Ushindi wa rais kenyatta baadaye ulitupiliwa mbali na mahakama ,ingawaje alishinda uchaguzi wa marudio ambao upinzani ulisusia .
Akombe, kupitia msururu wa jumbe za twitter ameiweka IEBC katikati ya mauaji ya Msando akisema wenzake ndio waliomsaliti kwa waliotekeleza mauaji yake .amesema yuko tayari kusema anachofahamu .
Alitorokea Marekani akihofia usalama wake na akarejea kulifanyia kazi shirika la umoja wa mataifa nchini humo .
“… Ni uchungu kwamba siku kama hii miaka mitatu iliyopita wenzako walikupeleka kichinjio .kama Judas walikuuza kwa senti 30’ Akombe aliandika katika twitter .
“ Tutahakikisha tunapigania haki yako na tuipate hata iwe muda gan’ alizidi kuandika .
Lakini mwenyekiti wa IEBC wAfula Chebukati amesema sio haki kwa Akombe kuzungumza sasa miaka mitatu baadaye ilhali alikuwepo wakati Mauji hayo yalipotendeka .
" Sote tunataka kuona haki ikitendeka kwa familia ya Msando .tumesema hilo kuanzia mwanzo’ Chebukati aliliambia gazeti la The Star
Akombe anaafa kuzisaidia maamlaka kufahamu ukweli kuhusu mauaji ya Msando .
" Yaonekana kuna jambo analofahamu ambalo wengine hatujui .Naamini hili linafaa kutoa habari za kutosha kwa idara za uchunguzi .Labda huenda habari hizo zitasaidia kukamilishwa kwa uchunguzi’ Chebukati amesema
Ameongeza kwamba IEBC imekuwa ikifanya kila jambo inaloweza kupata ukweli kuhusu mauaji ya Msando .
Chebukati amesema iwapo Akombe hawezi kujiwasilisha kwa DCI basi mipango inaweza kuwekwa ili maelezo yake yachukuliwe akiwa Marekani .
Akombe amekishauri chama cha wanasheria nchini LSK kuchukua kesi hiyo na kuifikisha kortini kwa maslahi ya umma na yuko tayari kutoa ushahidi .
Lakini Rais wa LSK Nelson Havi amepuuzilia pendekezo hilo .
“ Mimi ni DCI? Sifanyi uchunguzi wa mauaji.waulize watu wanaoshughulikia mambo kama hayo’ alisema