Sababu za mimba za mapema kwa wasichana wa shule barani Afrika

Ni swali ambalo wengi wanaulizana hasa wakati huu wa janga la corona si wakati huu tu pekee bali katika Afrika wasichana na wanafunzi wengi ukatizwa masomo yao kwa ajili ya mimba za mapema.Ni jambo ambalo limekuwa kizungumkuti kwa zazi wengi barani Afrika.

Swali kuu ni nini haswa husababisha mimba za mapema Afrika nzima je wakulaumiwa ni wasichana, wapenzi wao au wazazi wao?

Husitie hofu majibu yako yote utayapata hapa kutoka kwa makala haya, ya kwanini mna mimba za mapema Afrika? mimba za mapema bado zimesalia kuwa changamoto kubwa kwa wazazi.

Katika nchi yetu wasichana wengi wakifikisha umri wa ujana wao, asilimia 3% ya wasichana wa miaka 15 upata mimba wakati ujana wao huku asilimia hiyo ikizidi kuongeza huku 40% ya wasicha wa miaka 19 wakipata mimba za mapema.

Kati ya wanawake 1000, wasichana 96 upata mimba za mapema kila mwaka humu nchini.

Hizi hapa sababu za wasichana wengi kupaa mimba na kuacha shule;

1.Kutimiza mahitaji yao

Wasichana wengi hujiusisha na mapenzi ya mapema ili kutimiza mahitaji yao, kama vile kununua sodo kwa maana wazazi wwao hawana pesa za kununua wala kuwatimizia hitaji hilo.

2.Dhuluma za kijinsia

Si mmoja wala wawili bali wasichana wengi hupata mimba za mapema kwa maana wamedhulumia kijinsia, aidha na baba mzazi, ndugu au mpenzi wake hata mjomba wake.

Kisha wana jipata na mimba bila kujua chochote wala lolote.

3.Ukosefu wa habari kuhusu ngono na haki zao

Wazazi wengi hujipata wameshikana na kazi na kuwatafutia wanao riziki ya kila siku huku wakisahau kuwa wanajukumu la kuwafunza wasichana wao kuhusu ngono na haki yao kama wasichana

4.Udanganyifu kutoka kwa wapenzi wao

Wengi hujihusisha na ngono kwa maana wanawapenda wapenzi wao ilhali mwanamme huyo hana shughuli na msichana huyo bali anataka tu kumtumia na kumcheza kwa maana hana habari zozote kuhusu mapenzi.

Swali nije kwanini wajihusishe na mapenzi wanagali shuleni, kwa sababu umemuona mwenzia na mpenzi pia nawe wataka kuwa na mpenzi na kisha kujipata pabaya huku tayari una mimba na kutoka shuleni bila kumaliza masomo yako na kisha maisha yako kugeuka kwa sekunde moja.

5.Ndoa za mapema

Utampata mwanafunzi wa darasa la saba tayri ni mke wa mtu kwa sababu ashaatozwa na wazazi wake huku wakiogopa majukumu ya msichana wao.

Si kupenda kwa msichana huyo kuolewa mapema bali amelazimishwa na wazazi wake kufanya hayo na mwishowe kujipata hana mum wala baba wa watoto wake kwa maana tayari mwanamme huyo amepata mwingine na mwenye masomo.

6.Shinikizo ya kijamii ya kuoa na familia

Si wote wanapenda kuwa wake za watu au kuitwa mama kwa mapema lakini kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa jamii na hata jamaa zao wanajipata tayari wamebeba mimba na kuwalea wana wao pekeyao kwa maana mumewe tayari amemuacha na kuoa mwingine.

7. Mitandao ya kijamii

Kama sisi sote tunavyo jua na kufahamu karne hii ta sasa imebadilika na hata kisasi kubadili mienendo yao, utapata mtoto wa kiaka nane tayari ana simu anajua mitandao ya kijamii na wala mzazi wake hafuatilii nini haswa inachofanyika katika mitandao hiyo.

Endapo atawaona wanandoa wawili wako sawa na kamili akili yake inaona pia naye anapaswa kuwa hivyo na mambo ya masomo yanasahulika.

8.Dawa za kulevya na pombe

Endapo wasichana wengi watajihusisha na pombe na dawa za kulevya wakiwa kwenye ujana wao, huku wakijipata kwenye hali ya kulewa na kujihusisha na ngono mwisho wa siku watajipata na mimba na kuacha masomo yao

9.Wakati na wazazi wao

Wakati huu na karne hii wazazi wengine wamo kwa harakati zao za kutafuta riziki, lakini hawatengi wakati wao kuwa na wasichana wao na kuwauliza jinsi wanaendelea katika ujana wao.

10.Umaskini

Ni matamanio ya kila msichana apate atakacho na kuona familia yake hiko tayari kumsaidia na chochote kama vile marafiki zake, kwa kweli huwa wanajihusisha na ngono za mapema ili kupata pesa na kutimiza mahitaji ya familia yake.

Je wa kulaumiwa kwa sababu ya mimba za mapema ni nani na kwanini,kwa kweli wa kulaumiwa ni wazazi wasichana na wapenzi wao wote ni wakulaumiwa kwa ajili ya kitendo hicho.

Kama mzazi unapaswa kujua nini haswa kinaendelea  katika maisha ya mwanao na nini kinamsumbua kama msichana, lakini si wote ambao wana wakati huo.

Pia kama msichana unapaswa kujua jukumu lako na nini unapaswa kufanya, pia wahitaji kujua thamani yako katika maisha yako na wala si kila mara kushiriki ngono na mwanamme ambaye unapata kwa njia wala amekuongelesha ili uwe mpenzi wake.

Wasichana pia wanapaswa kujua kuwa si vyema kuwa na mpenzi hasa ukiwa shuleni kwa maana kimoja kitaungua na kile cha muhimu ndicho kitaungua na kuwa na hati ya ujauzito badala ya masomo yako.

Wapenzi wao pia ni wa kulaumiwa, kwa maana kwa kweli wanajuwa huyu ni mwanafunzi lakini nia yake ni kuharibu maisha ya mtoto huyo na mwishowe kumuacha ili ang'ang'ane na kumlea mtoto pekee.

Wengi si wapenzi wa shule bali mwanamme ambaye anajua ubaya na uzuri, ni mwanamme ambaye ana umri zaidi lakini hana mawazo ya kuwa huyu msichana ni mwanamfunzi.

Wazai pia wanapaswa kuwapa elimu kuhusu ujana wao wanachoctahili kufanya na wasiostahili kufanya kama msichana.

Si mmoja au wawili bali wasichana wengi wameacha shule kwa ajili ya mimba za mapema, kulingana na wazazi wengi wao hawana makosa kwa wasichana kubeba mimba bali hawajawahi kuwafunza madhara ya mimba za mapema.

Ni kweli wanafunzi wengi muda wao mwingi wanakaa na walimu na wala si wazazi wao, wakati huu wa janga la corona tumeshuhudia wasichana wengi wakiwa wamepata mimba za mapema,ina maana kuwa wazazi wamesahau majukumu yao au mambo yako vipi?

Au ina maana wasichanaa hao wamesahau na majukumu ya kusoma na kujihusisha na ngono au wazazi wamewapa nafasi nyingi ya kutenda mambo yasiostahili?

Ni swali ambalo litazidi kugonga kwenye vichwa vya wananchi wengi huku wakiulizana nani wa kulaumiwa kwa mimba za mapema ambazo zimeuwa changamoto nyingi katiia karne hii, kwa maono yangu mimi hamna mtu yeyote wa kulaumiwa kwa maana kila msichana ana habari kuhusu ngono na anajua jukumu lake kama mwanafunzi ni kusoma hamna la kuongeza wala kugawa.

Pia wanafahamu mapenzi ya mapema kwa kweli yataharibu maisha yao na ndoto zao kuziwa mapema, lakini nani wa kulaumiwa kwa ajili ya mimba za mapema?

Je tutakomesha vipi mimba za mapema na juhudi zipi ambazo zinapaswa kutumiwa ili kukomesha kitendo hicho? Je maoni yako ni yapi kuhusi mimba za mapema na nani wa kulaumiwa?