Akombe, wiki jana alikuwa amefichua kwamba Msando ambaye alikuwa maneja wa ICT wa tume hiyo alielekezwa ‘kichinjio’ na watu wlaiokuwa wakifanya kazi katika tume hiyo .
Alisema yuko tayari kutoa ushahidi endapo jopo la uchunguzi litaundwa kuchunguza mauaji ya Msando .
Siku ya juapili alitumia twitter kuchapisha parua pepe ambayo amedai Chiloba alimtumia akimtaka anyamaze kuhusu hatuayake ya kutaka kufichua anayojua kuhusiana na mauaji ya Msando .
" Usiandike upya historia .unyamavu wetu sio leseni kwako’ ilisema barua pepe hiyo iliyoandikwa na Chiloba
Akombe amesema vitisho vya Chiloba ni dhihirisho kwamba mauaji ya Msando yalikuwa kazi ya ‘wandani’ katika tume ya IEBC
" Inathibitisha kwamba panahitajika kuwa na jopo la uchunguzi .Wakenya wanastahili kuambiwa ukweli’ Amesema Akombe .
Hata hivyo Chiloba ambaye anafanya ukulima baada ya kuondoka IEBC mwaka wa 2018 hakuthibitisha kutuma au kukana kuituma barua pepe hiyo .
“Really? No comment,” Chiloba alisema kupitia ujumbe mfupi kwa gazeti la The Star alipoulizwa kuhusu parua pepe hiyo .
Akombe, aliutangaza julai tarehe 30 kwamba yuko tayari kutoa ushahidi mbele ya jopo la uchunguzi endapo litaundwa kung’amua ukweli kuhusu mauaji ya ChriS Msado .