Msanii Rich Mavoko arejea tena kwenye tasnia ya usanii

Msanii wa nchi ya Tanzania Richard Martin almaarufu Rich Mavoko amerejea kwenye usanii wake na hata kwenye mitandao ya kijamii baada ya takriban miezi kumi na moja.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii Mavoko amesema kuwa atatoa nyimbo zake kadhaa Agosti,8, ili avunje kimya chake cha muda mrefu.

“I MISSED ALL MY PEOPLE. Just keep the date on your mind. .

Kwenye Youtube Mavoko anafahamika kama Messi of Bongo Flavour, alitoa wimbo wake wa mwisho mwaka jana Agosti,29.

Mei mwaka huu msanii Harmonize alionyesha uhusiano wake kuhusu Mavoko huku akidai kuwa alikumbwa na matatizo baada ya kutoka katika lebo ya WCB.

“Mana Mzazi wa Mwenzio Ni wako Pia Laana Yake Haishindwi Kukupata ...!! La Mwisho Kabisa Mgeukie Mwenzio Anaefurahia Na Kuifanya Hii Kuwa Ni Habari Njema Kwake Ya Kumfanya Atembee Kifua Mbele Na Hata Kuandika Mtandaoni Kwa Furaha MAVOCO KAPOTEA muulize Anafaidika Nanini ...??? Mungu Anasababu Na Maana Yake Bro Kama Mdogoako Nakuombea Najua Ukimya Wako Unamaana Kubwa Sanaa Ndani Yako Ninachojua Ni Kujiweka Sawa Na Kutuletea Kazi Zingine Tunakupenda Na Tunakuombea Mungu Akufanyie Wepesi...!!! Let's Go Bro Mdogoako Rafiki Yako Nipo Hapa Muda Wowote...!!!! RAMADAN KAREEM."

Mavoko alitoka katika lebo ya WCB mwaka wa 2018, Julai.