Afisa mkuu mtendaji wa hazina hiyo Peter Kamunyo aliambia meza yetu ya habari kuwa asilimia 77 ya watu binafsi waliokuwa wakichangia bima hiyo shilingi 500 kila mwezi wamesitisha mchango wao.
Soma habari zaidi;
Wengi wanaochangia hazina hiyo ni wale waliyojiajiri na wenye biashara ndogo ndogo ambazo huenda ziliporomoka kutokana na athari za janga la corona na kufungwa kwa shughuli za kawaida nchini na kimataifa.
"Hii ni kufikia mwisho wa mwezi Juni. Malipo ya hazina kutoka kwa watu walioajiriwa pia yameshuka kwa kiasi fulani," alisema.
Hazina hiyo ina wanachama milioni 8.5 lakini kwa sasa ni milioni tano pekee wanaolipa.
Watu wengi katika mpango wa watu binafsi kujilipia walikuwa tayari wameanza kuacha kulipa hata kabla ya janga la virusi vya corona, ni asilimia 35 pekee waliokuwa wakilipa vyema.
Soma habari zaidi;
Alisema mpango huo hauwezi kujisimamia kwa sababu NHIF hugharamia mara tatu zaidi malipo ya matibabu ya wakenya chini ya mpango huo.
Kamunyo alikuwa akizungumza ofisini mwake baada ya kutia saini makubaliano na kaunti ya Kisumu kulipia wenyeji bima ya matibabu.
Soma habari zaidi;
Kaunti hiyo itatoa shilingi milioni 22.5 kulipia bima za matibabu familia 45,000 kuambatana na makubaliano yao.
"Hawa ni watu ambao hawawezi kumudu kulipia bima za matibabu. Tuliona tuwasaidiye kupata huduma za matibabu," naibu gavana wa Kisumu Mathews Owili alisema.
"Kila familia ina takriban watu wanne, kwa hivyo idadi hii ni kama watu laki mbili".