Kiongozi wa chama hicho Raila Odinga siku ya Jumanne aliifurusha bodi ya zamani ya uchaguzi iliyokuwa ikiongozwa na Judy Pareno na ambayo ilishtumiwa kwa kusimamia vibaya mchakato wa uchaguzi wa kuwateua wagombeaji wa ODM na kuvuruga matokeo ya chama katika uchaguzi mkuu uliopita
Catherine Mumma aliywahi kuhudumu katika tume iliyovunjiliwa mbali ya utekelezaji wa katiba sasa ndiye mwenyekiti mpya wa bodi ya kitaifa ya uchaguzi . wengine katika bodi hiyo ni mbunge wa zamani wa wajir kusini Abdulahi Diriye, Richard Tairo, Syntei Nchoe na Emily Awita.
Prof Ben Sihanya anachukua usukani kama mwenyekiti wa kamati ya nidhamu kutoka kwa wakili Fred Athuok. Kamati hiyo ya nidhamu pia ina sura mpya kama vile Ramadhani Abubakar, Mumbi Ngaru, Seth Kakusye na Dr Florence Omosa.
Hatua ya Raila kumteua Mumma katika bodi ya uchgauzi inalenga kutumia ujuzi wake katika sheria kutekeleza ripoti ya tathmini yenye mapendekezo mengi ya kuboresha matokeo ya uchaguzi ya chama hicho .
Mumma aliongoza kamati iliyotoa mapendekezo na kuikosoa vikali bodi ya zamani kwa kutumia ghasia ili kuwapa vueti wagombeaji ambao hawakuwa na umaarufu mashinani .
Bodi hiyo mpya itatoa ratiba na kuandaa uchaguzi wa chama hicho ambao uliahirishwa kwa sababu ya janga la Covid 19