Mr President:Mvulana mwenye umri wa miaka 19 kugombea urais Uganda

hillary
hillary
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 19 nchini Uganda amechukua fomu kugombea kiti cha urais wiki hii.

Kijana huyo kwa jina Hillary Humphrey Kaweesa ambaye ni muhitimu wa kidato cha sita mwaka jana,alichuwa fomu za kugombea katika ofisi za Tume ya Uchaguzi nchini humo.

Kaweesa anasema ameamua kuchukua fomu kwa kuwa ana vigezo vinavyomuruhusu kugombea kiti hicho.

"Nina umri wa mika 19 nimehitimu kidatu cha sita katika shule ya upili ya Mengo, na nimeamua kugombea kiti cha urais wa Uganda. Mimi ni mjukuu kwa yule ninayeshindana naye , nina vigezo vya kugombea kiti hicho kwani mimi ni raia wa Uganda, nina uzoefu nimekuwa kiongozi katika shule na ndoto yangu ilikuwa ya kugombea nafasi ya juu na sasa nimefanikiwa,"alisema Kaweesa.

Kugombea kiti cha urais nchini Uganda unatakiwa kulipa ada ya shilling milioni 20 za Uganda ambazo ni sawa na dola $5400, kiasi ambacho Kaweesa amesema anatarajia kupata fedha hizo kutoka kwa wasamaria wema nchini humo.

Kila mgombea wa kiti cha urais anatakiwa kuugwa mukono na watu 100 watakaoweka sahini kwenye fomu yake suala ambalo halimpi hofu kwa kuwa anadai kuwa na watu wengi zaidi ya idadi hiyo.

Tangu Katiba ya Uganda iipofanyiwa marekebisho ya kuondowa umri wa mgombea wa kiti cha urais na kikomo cha miaka 75, mtu yoyo aliye na umri wa kuanzia miaka 18 anaruhusiwa kugombea .

Mpaka sasa rais Yoweri Museveni ameshahidhinishwa na chama chake kutetea kiti chake naye msanii Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine akipeperusha bendera ya vuguvugu la People Power huku Jenerali Henery Tumukunde alitangaza kama mgombea wa kujitegemea na wengine wengi wakiendelea kuchukua fomu.