Jinsi msanii wa WCB Mbosso alivyopoteza shilingi milioni 100

Staa wa Bongo Mbosso  ameathiriwa pakubwa na janga la corona kama wasanii wenzake atika fani ya muziki kwani anasema amepoteza takriban shilingi milioni 100  kwa ajili ya kupoteza  biashara kutokana na hali ilivyo sasa .

Mbosso amesema amelazimika kuziacha show kadhaa na kwa jumla angelipwa kati ya shilingi milioni 80 na 100 za Tanzania endapo angezipisha show hizo .

 Nilikuwa na show kadhaa  za kupiga na pia nilifaa kufanya ziara ya kwenda ufaransa . yote haya yalifaa kufanyika mwezi aprili lakini sasa hakuna njia nyingine vitu vimesimama

Diamond awali pia amedai kwamba amepoteza  takriban shilingi bilioni 3 za Tanzania ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 100 za Kenya .