Usikubali hawa ministers wakuharibie jina-Gavana Sonko amwambia Uhuru

mike sonko
mike sonko
Gavana wa kaunti ya Nairobi Mike Sonko alithubutu kumwambia rais Uhuru Kenyatta maneno nadra sana akiwa kwenye mahojiano  alimwambia Uhuru kwamba ang'ang'ane na jambo ambalo linaitwa 'system' huku akiwa amewaamini waziri Fred Matiang'i na Karanja Kibicho.

Huku akimhutubia rais alisema kuwa kazi ya ikulu ni kama 'ujinga' na anapaswa  kutumia kiboko chake.

"Rais Uhuru, ndugu na rafiki yangu usikubali hii ujinga ifanyike kuna methali ambayo inasema kama baba kama mwanawe baba yako angewaita wahudumu wenye tabia mbaya na kuwacharaza viboko

Usikubali hawa ministers wakuharibie jina wakenya wanakupenda sana lakini huu ukora inaendelea."

Akizidi na mazungumzo yake Sonko alida kuwa Uhuru amerudisha nchi nyuma kwa ajili ya unyanyasaji na vitisho  vya polisi.

"Systen ni Matiang'i na Kibicho alafu ikulu, waziri Matiang'i ni mzuri kwa kazi yake lakini shida ni pale anatumia mamlaka vibaya kama vile ilivyowatendekea maseneta

Hii ilikuwa kazi ya Matiang'i na Kibicho na siwaogopi kama vile watu wengi wanawaogopa, wanaweza nitimua afisi kama wanataka , ukweli ni kuwa nimemjua rais kwa muda mrefu na amri hiyo haukutoka kwake bali kwa watu wengine

Kuna watu ambao wamemzunguka ambao ndio shida." Alizungumza Sonko.

Sonko alirudia kuwa alikuwa amelewa alipokuwa anatia saini majukumu ya kaunti ya Nairobi na kupa serikali kuu.