‘Ambieni hio panya nono ipunguze matumbo…’ Octopizzo amkejeli Khaligraph Jones

Inaonekana kuwa kuna ugomvi umetokea au unatokea kati ya rapa wawili Khaligraph Jones na Octopizzo ambao wanafahamika sana humu nchini.

Awali wawii hao walikuwa na ugonvi huku Khaligraph akimuomba Octopizzo washirikiane katika kibao kimoja.

"Na mi sina beef na Ohanga. Ohanga hunitaki kwa nini, mbona usifanye track na mimi tu top hizi charts za Mjini, after that I would be happy amini. Sitaki interview za gazeti , maswali za ufala hazileti , mimi huomba kama ndingi wa Nzeki, GOAT kama Ronaldo na Messi, nani mwingine kama mimi (hakuna), mafuta napaka Marini…"

Hivi juzi Jones ametoa kibao ambacho kinafahamika kama 'Lwanda magere' na kulingana na Octopizzo wimbo huo haujaweza kwa maana hajamtaja katika kibao hicho.

Ilianza pale Jones alimwambia Octopizzo aache kuongeza mambo ambayo hayastahili katika mitandao yake ya youtube huku mashabiki wengi waisema kuwa mashabiki wake Jones wameanza kupungua huku wengi wakisema kuwa Octopizzo amenunua mashabiki hao.

Usemi wake Khaligraph haukupokelewa vyema na Octipozzo ambaye alijitokeza akiwa ameweaka moto na kusema,

"KUNA NGOIMA FLANI TANGO IANZE KUDOZ NA POINTI AMECHANGANIKIWA, PEREKA HIZO MIXED FEELINGS KWA BEDROOM NANI. AMBIENI HIO PANYA NONO IPUNGUZE MATUMBO KWANZA NDIO INIONGELESHE, ACHA KUNITAJATAJA MSE. NGOMA ZAO HAZITREND BILA DON KWA MENTION 😂😂

EKA FAMILIA YOTE IG NDIO NGOMA ISONGE NANI ☠️ “WAMESHONA LAKINI MI NDIO TAILOR MEN!”

Je hii drama nyingine ambayo wamezua huku wakitaka mashabiki watazame nyimbo zao?