'Wacha kufikiria na kichwa chako cha chini,' Babu Owino amwambia Miguna

IiRk9kpTURBXy9hZWI0MTdmY2M0NDAyZTRkNWIyNDQzYjhjY2Q4OTQ0Mi5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB
IiRk9kpTURBXy9hZWI0MTdmY2M0NDAyZTRkNWIyNDQzYjhjY2Q4OTQ0Mi5wbmeRkwXNAxTNAbyBoTAB
Cheche za maneno zimeshuhudiwa Jumanne kwenye mitandao ya kijamii ya twitter kati ya mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino na wakili Miguna Miguna.

Majibizano yao yalianza pale Miguna alimshirikisha Babu na mauaji ya Kevin Omwenga aliyepigwa risasi akiwa nyumbani kwake Kilimani Jumamosi iliyopita.

"Hooligan washirika wa jinai wa mbunge Babu Owino walimuua Kevin Omwenga kwa ajili ya mikataba ya dhahabu bandia haya yalikuwa mauaji ya 13 yao kutekeleza lakini walinzi wao Raila Odinga, Fred Matiang'i, Moses Wetangulam na Roda Omamo hawajakamatwa." Aliandika Miguna.

Baada ya mbunge huyo kuona ujumbe huo alimpa bonge la jibu na kusema;

"Miguna Miguna wacha kufikiria na kichwa chako cha chini hakina akili." Alijibu Babu.

Ni jibu ambalo liliibua hisia mseto kwenye mitandao hiyo huku wengi wakimshauri hasichukulie jambo hilo au matamshi hayo kwa makini.