Uhuru atuma rambirambi zake kwa Aden Duale baada ya kumpoteza mama yake

Aden Duale
Aden Duale
Rais Uhuru Kenyatta ametuma risala za rambirambi kwa familia ya mbunge wa Jiji la Garissa Aden Duale baada ya kumpoteza mama yake.

Duale alimpoteza mama yake Mama Hawa Jumanne huku rais akijiunga na waombolezaji kwa kutumba risala zake kwa famili ya mbunge huyo.

Rais alimuomboleza Mama Hawa Kosar kama mwanamke mnyenyekevu, mwenye bidii na mwenye kujitolea katika kazi za Mungu, huku akisema maneno na ushuri wake wenye maarifa utapezwa maishani.

Chama cha Jubilee pia kilituma risala za rambi rambi zao kwa familia ya Duale na kuandika ujumbe ufuatao;

"Chama cha Jubilee kinajiunga na familia ya mbunge wa jiji la Garissa Aden Duale kuomboleza kifo cha mama yake Mama Hawa Kosar Shaurie

Wacha Mungu aijaze familia hiyo na nguvu wakati huu wamekabiliwa na kifo cha mama yao,Mama Hawa Kasor lala mahala pema peponi." Ujumbe ulisoma.

Pia naibu rais William Ruto alimkumbuka mwendazake kama mwanamke wa dini aliyejitolea na amabaye alilea watoto wenye bidii.

"Rehema zetu za moyono zinawaendea familia na mbunge wa Garissa Aden Duale kwa kumpoteza mama yao mzazi, Mama Shaurie alikuwa mwanamke wa dini aliyepewa heshima na aliyekuza na kuwalea watoto wenye bidii licha ya kuwa na changamoto." Aliandika Ruto.

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.