'Murkomen anza kujipanga kuondoka,'Waziri Tobiko aapa kumfurusha Murkomen

tobiko
tobiko
Vita za cheche za maneno kati ya seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen na waziri wa mazingira Keriako Tobiko zinazidi kuchacha na kushuhudiwa kila kuchao.

Mnamo Septemba,5,Tobiko alidai kuwa Murkomen ni miongoni mwa watu ambao wanaishi katika msitu wa Embombut na hivi karibuni atamfurusha kutoka maeneo hayo.

Pia alidai kuwa Murkomen alipinga zoezi la kuwahamisha watu katika msitu wa Mau.

Wawili hao wamekuwa kwenye cheche za maneno baada ya Tobiko kumuita Naibu Rais William Ruto kama karani tu kwenye serikali.

"Hatutakubali yale yalifanyika msitu wa Mau. Wakati watu walikuwa wakitolewa Mau Murkomen alikuwa mmoja wale wale walipinga zoezi hilo

Yeye anaisha msitu wa Embombut. Murkomen anza kujipanga kuondoka." Tobiko Aliongea.

Baada ya matamshi yake Tobiko Murkomen naye alisema kuwa hatishwi na usemi wake Tobiko huku akidai waziri huyo anataka kulipiza kizazi kwake na kwa baba yake.

"Tuna waziri ambaye ana utoto, Yaani kwa sababu ya ujumbe wa twitter ameamua kulipiza kisasi kwangu na babangu," alisema Murkomen."Aliongea Murkomen.

Je cheche hizi za maneno zitashuhudiwa hadi lini kati ya viongozi hao wawili?