'Si ngono bali ni maarifa katika uhusiano,'mumewe msanii Vivianne amtetea Guardian Angel

Siku chache baada ya msanii wa nyimbo za injili Guardian Angel kumtambulisha mpenzi wa maisha yake ambaye ana miaka hamsini mengi yamesemwa na hata maoni mengi yakatolewa na wakenya.

Mumewe msanii Vivianne Sam West amemtetea msanii huyo huku akitumia vifungu vy biblia.

Kupitia kwenye mitandao yake ya kijamii ya instagram Sam West alikuwa na haya ya kusema;

https://www.instagram.com/p/CE3TVGSJkPn/

"Wengi wenyu wamekuwa wakiniuliza nijibu swali la je ni sawa kuoa mtu ambaye ana umri mkubwa kukushinda, huwa najibu kulingana na neno la Mungu

Biblia haijazungumzia mahitaji yeyote ya ndoa hasa umri, hata hivyo naweza kusema kuwa watu wawili wanapokuja pamoja hiyo ni historia inakuja pamoja

Mtu ambaye ana miaka 50 na kisha aoe mpenzi wa miaka 50 hiyo ni historia mia moja zimekuja pamoja katika kitanda hicho, historia inakuja na kutoka kwa uhusiano wa awali,familia watoto, kuumizwa moyo." Alieleza Sam.

Sam alisema ya kuwa ili ndoa iweze kudumu kuna mambo matatu muhimu ya kuzingatia kama vile kuelewana, maarifa na hekima na kisha kuandika kitabu cha (mithali 24:3).

"Si kuhusu upendo ama ngono, ni maarifa na habari kuhusu vile uhusiano unaendelea kuelewa jinsi vile upendo hufanya kazi na hekima ni moja wapo wa maarifa ya uhusiano."