Covid-19:Watu 183 wapatikana na corona huku idadi ikifika 36,576

Kenya hii leo imesajili visa 183 mpya vya maambukizi ya corona na kufikisha idadi ya 36,576 watu walioambukizwa corona hii ni kutokana na sampuli 4,188 zilizopimwa ndani ya saa 24 zilizopita.

Katibu msimamizi wa wizara ya afya Mercy Mwangangi amesema ya kwamba Watu 5 wameaga dunia kufuatia kutokana na virusi vya corona na idadi ya jumla ya waliofariki kufikia watu 642. 82 wamepona na wote waliopona ugonjwa huo wamefika watu 23,611.

Pia amesema kuwa wahidumu wa afya 945 wameeta maambukizi ya corona huku 16 wakipoteza maisha yao tangu maambukizi ya corona yaanze kurekodiwa nchini.