logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Tunahitaji pesa na msaada wa Ruto,makasisi na wahubiri wasema

Tunahitaji pesa na msaada wa Ruto,makasisi na wahubiri wasema

image
na

Habari01 October 2020 - 09:27
KASISI
Baadhii ya  makasisi na wahubiri kutoka North Rift wanamunga mkono uhusiano wa karibu wa naibu wa rais na  kanisa kwa sababu ya msaada wake na pesa wakisema wanazihitaji .

Wakiongozwa na  Askofu  Simon Kemei  wamesema pesa zozote zinazopewa makanisa zimetakaswa bila kujali zilizkotoka .

Kimei siku ya jumanne amewapuuza wanaopinga hatua ya Ruto kuwa mkarimu kwa makanisa  na kumtaka Ruto kuyasaidia makanisa yote  yakiwemo katika eneo la North Rift .

Ruto  amekuwa mkarimu kwa makanisa na viongozi wa kidini huku misaada yake pia ikiwafikia vijana na makundi ya akina mama ili kuwekeza katika miradi ya kujipata mapato

“ kama viongozi wa kidini tumefurahi sana na anachofanya naibu wa rais kuyapa misaada makanisa  na tunaamini anatumiwa an Mungu kuwasaidia watu wanaohitaji msaada wake’ amesema Kemei

Alikuwa akizungumza huko Eldoret baada ya maombi ya mkutano wa maombi ya  wiki nzima. Makanisa yana mahitaji mengi na DP ameyasaidia sana ,amesema Askofu huyo .

“ Iwapo naibu wa rais atakuja katika kanisa langu nitafurahi sana kumpokea kwa moyo wote  .kama kiongozi wa waumini wangu najua hatuna ala za muziki ,viti  na tuna mahitaji mengi ambayo naibu wa rais anaweza kutusaidia’ amesema

Matamshi yake yalikaririwa pia na Askofu  John Korir  a mhubiri  Joseph Too . Wamesema wale wanaomshtumu Ruto kwa ufisadi hawana uwezo wa kumtolea hukumu na badala yake wanafaa kujiunga naye kuifanya kazi ya Mungu .


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved