Kila mtu ni mshindi! Ruto apongeza seneti kwa kupitisha msuada wa mgao wa mapato

Naibu rais William Ruto amepongeza seneti kwa kuafikiana na kupitisha mfumo wa ugavi wa mapato kwa serikali za kaunti.

Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa Twitter naibu rais alisema kwamba mfumo uliopitishwa na maseneta ni bora na utahakikisha kwamba kuna usawa kwa kila mtu kwani hakuna kaunti itakayopoteza pesa chini ya mfumo huu mpya.

Alisema njia ya pekee ya kufanikisha jambo inafaa kuwa kupitia mazungumzo yenye busara na sio kupitia vitisho.."REASON not intimidation" Ruto alisema kwenye ujumbe wake.

Maseneta 41 siku ya alhamisi walipitisha mfumo utakaotumiwa kuzipa fedha kaunti baada ya miezi kadhaa ya utata.

Maseneta hao walipitisha kwa kauli moja ripoti ya kamati maalum ya maseneta 12 waliokuwa wamepewa jukumu la kuafikia mfumo ambao utakubaliwa na kaunti zote .

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ameahidi kuzipa kaunti shilingi bilioni 50 katika mwaka ujao wa kifedha na kurahisisha kazi ya kupatikana kwa mwafaka wa kukubaliwa na wote.

Kakamati hiyo ilisimamiwa kwa pamoja na maseneta Johnson Sakaja na Moses Wetangula ndio iliyoafikiwa mfumo huo .

Mfumo huo uliopendekezwa unatilia mkazo vigezo vinane mgao wa mwanzo(asilimia 20) idadi ya watu(asilimia 18) afya (asilimia 17) kiwango cha umaskini(asilimia 14) kilimo(asilimia 10) barabara(asilimia 8,ardhi (asilimia nane) na miji(asilimia tano)

Katika mfumo mpya Nairobi ndio itakayopewa mgao wa juu wa shilingi bilioni 18 baada ya kupewa bilioni 3.3 za ziaa .kaunti nyingine zenye migao ya juu ni Nakuru (Sh2.5 billion), Kiambu (Sh2.2 billion) na Turkana (Sh2 billion).

Mgao wa Lamu umeongezeka hadi shilingi bilioni 3.1 ilhali Tharaka Nithi imeongezwa shilingi milioni 289. Hakuna kaunti inayopoteza pesa katika mfumo huo mpya.

Soma habari zaidi hapa;