'Nimeambia familia yangu nikifa wanizike siku hiyo,' Akothee

Msanii Esther Akoth almaarufu Akothee amefichua kuwa ameuliza familia yake imzike siku ambayo ataaga dunia na wala si siku ifuatayo.

Akiandika hayo kwenye ukurasa wake wa instagrama Akothee alisema kwamba hataki kupitia magumu ambayo mama yake amepitia kwa mwezi mmoja huku akingooja mke wa ndugu yake aweze kupewa heshima zake za mwisho.

Akothee aligadhabishwa na vile watu wanampigia simu aweze kutoa mchango wa mazishi yao ilhali hamna mtu mmoja ambaye ameweza kumuuliza mkewe ndugu yake atazikwa lini.

https://www.instagram.com/p/CFQxLE-nEmE/

"Watu wengine bado wananitumia jumbe na hata kunipigia niweze kuchanga kwa ajili ya mazishi yao hamna mtu yeyote ambaye ameniuliza kunipeleka kwenye mazishi wala kuniuliza mazishi yako siku gani

Wakati huu sina nguvu ya kumuangalia ndugu yangu akimteremesha mke wake kwenye kaburi sijui niweke kichwa wapi?

Kwangunmimi nikifa leo nimeuliza familia yangu inizike siku hio hio, kiwewe ambacho mama yangu amepitia kwa mwezi huu mmoja akingoja nyabondo kwa ajili ya hali ya covid siweze muona akienda kwenye mazishi

Wacha Mungu akajaze kila familia iliwapoteza wapendwa wao wakati huu mgumu." Akothee Aliandika.