PATANISHO:Baba mkwe alichukua mke wangu ampeleke chuo kikuu hajawahi rudi

David Gitai,31, Alituma ujumbe apatanishwe na mkewe,Virginia waliokosana mwaka jana baada ya wazazi wake kumtoa kwenye ndoa na kudai wanampeleka chuo kikuu.
"Baada ya kufahamu hayo nilienda kwao nikiwa nimebeba bidhaa tofauti na elfu kumi, baba mkwe alichukua bidhaa hizo na kuniregeshea na hata kuwanayang'anya wanangu peremende nilizokuwa nimewanunulia

Sijui kama walidharau kazi yangu kwa maana kazi yangu ni ya kunyoa, nilienda huko alipochukua elfu kumi aliniambia kuwa hiyo ni ya kujua nyumbani kisha akaniambia niongeze elfu tano ili hasiweze kupeana mke wangu

Tulikuwa tunaishi vyema kwa miaka saba,nataka nirudishiwe bibi au pesa zangu ama watoto,nimeteseka sana ." Alieleza David.

Mkewe Virginia alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema,

"Nina lea watoto asiwe na shaka wala shida yeyote,kama anaumia basi atafute mtu mwingine wa kumsaidia, nilimwambia siku yenye atatoka kwa wazazi tutaskizana."

Kwa mengi zaidi tembelea mitandao ya youtube