'Sijawahi jua hatua waliochukulia askari walionidhulumu,' mwakilishi wadi Patricia Mutheu

Je wamkumbuka Patricia Mutheu Leo studioni zetu tulikuwa naye mwakilishi wadi huyo wa mlango kubwa, huku akizungumzia kisa chake cha kuchapwa na polisi alikuwa na haya ya kusema.
"Nilikuwa mahala pangu pa kazi, polisi waliwasili nilipowauliza nini walichokuwa wanafanya polisi mmoja alinipiga kofi na kuninyonga kisha kunitupanisha chini wale wengine walifuata na kuanza kunitandika

Baada ya kitendo hicho niliena kwa polisi kushtaki lakini polisi ni wengi ilhali madaktari ni wawili licha ya kuwa watu wengi wanaotaa haki

Nililazwa hospitali kwa maana niliumia sana kwenye mgongo wangu ambapo huwa nafanya zoezi kila siku na huwa nalipa, hadi waleo sijawahi jua polisi hao walichukuliwa hatua gani

Sikuwa katika mkutano wa kaunti nilikuwa nangoja rafiki yangu, nia ya polisi mmoja alikuwa anataka kunichapa teke kwenye uso wangu."

Huku akizungumzia jinsi familia yake ilichukulia jambo hilo alikuwa na haya ya kusema,

"Mtoto wangu wa miaka nane aliumia sana baada ya kuona kitendo hicho, lakini lazima apate ushauri kuhusu kitendo hicho."

Mwakilishi wadi alisema kuwa ni mchezaji kandanda ambaye alionelea ni vyema kujiunga na siasa ili kujua mengi.

"Nilijiunga na siasa bali sikuwa na mtu yeyote wakunielekeza, bali sijaona masuala ya vijana ikitekelezwa vyema na jinsi inavyostahili

Watu wengi hawatilii wadhifawa uwakilishi wadi maanani, kwa maana utapata mradi umekamilika kufanyika lakini malipo yamecheleweshwa sana."

Tembelea mitandao yetu ya kijamii ya youtube kwa uhondo zaidi.