Si mmoja au wawili bali mamillioni ya wanadamu wameachana kwa ajili ya kutoaminiana na hata kutojua ishara kama mwenzake anampenda au anamcheza na kuharibu wakati wake.
Si wote ambao ujihusiasha katika uhusiano wa kimapenzi kama amemchunguza mwenzake.Baada ya wengi kuwa katika uhusiano na kuwazoea wenzao huwa wanaanza kuwacheza na bila kujua unapata umeachwa kama mchezo wa paka na panya.
Hizi hapa baadhi ya ishara za kuonyesha kama mpenzi wako anakucheza na kuharibu wakati wako;
1.Ana hisia nyingi
Endapo umemkosea mpenzi wako hata kwa ndogo unapata amekasirika kupita kiasi na hata kukulaumu kwa kila jambo.
2.Kukupa zawadi nyingi na kukusifu
Ukiona mpenzi wako ghafla ameanza kukupa zawadi ambazo hukuwa unatarajia na hata ambazo hukuwa unapokea toka zamani basi jiulize swali kuna ni?
Si wote huwasifu wapenzi wao kupita kiasi kama wataka kufahamu mpenzi wako anakucheza haya basi ataanza kukusifu kwa vitu vidogo vidogo na visivyostahili.
3.Ana hairisha siku ya kukutana
Kama mlipanga siku ya kukutana na hata kukupeleka mkahawani kusherehekea uhusiano wenu ama kuonyesha upendo wake kwako, siku hiyo itakapofika ata ahirisha na kukupa sababu zisizostahili kumbe huenda ana mpango wake wa kando wanasherehekea.