Mpwa wake mtangazaji wa Radiojambo Ghost Mulee aaga dunia

Ghost-Mulee-mourning-Lawrence-Mbithi-1
Ghost-Mulee-mourning-Lawrence-Mbithi-1
Mtangazaji wa Radiojambo wa kipindi cha asubuhi Gidi na Ghost, na aliyekuwa kocha wa mpira wa kandanda Ghost Mulee yuko kwenye maombolezi hii ni baada ya mpwa wake kuaga dunia, Ghost alitangaza kifo chake kwenye ukurasa wake wa Instagram huku mashabiki wake wakituma risala za rambirambi.

Ghost kupitia kwenye ukuraasa huo alikuwa na haya ya kuandika,

https://www.instagram.com/p/CFbmYenDpZA/

"Mpwa wangi Lawrence Mbithi Musyoki 'Teddy' lala salama haijakuwa jambo rahisi kukubali kuwa sitawahi ona tabasamu yako tena, lala salama." Aliandika Ghost.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali  pema peponi,hizi hapa baadhi ya jumbe za mashabiki.

:Poleni sana
:Kazi ya mungu haina makosa mungu hutoa kisha hutwaa may he rest in peace
:May his soul rest in peace🙏